The Revolutionary Government of Zanzibar

News

Kamati ya Uchumi na Uwekezaji ya Baraza la Wawakilishi imeipongeza Kampuni ya Maendeleo ya Mafuta na Gesi Asilia Zanzibar ZPDC kwa hatua kubwa za Maendeleo katika Utafiti wa Mafuta na Gesi Asilia kwa njia ya mtetemo.

Kamati hiyo iliyofanya ziara ya ukaguzi wa utafiti huo unaoendelea katika Mkoa wa Kaskazini Unguja, imeonesha kuridhishwa na juhudi za ZPDC katika kuhakikisha inafikia malengo ya utafiti.

Aidha, changamoto mbalimbali zinazolikabili zoezi hilo zikiwemo za wananchi kutokutoa ushirikiano mzuri kwa kuharibu baadhi ya vifaa vya utafiti jambo ambalo linaweza kudhoofisha zoezi hilo muhimu.

Mwenyekiti wa kamati Mhe. Makame Mohammed Sufiani ameviomba vyombo vya ulinzi na usalama kuchukua juhudi za makusudi Ili kuokoa hasara kubwa itakayo jitokeza ikiwa vifaa hivyo vitaendelea kupotea na kuharibiwa jambo ambalo linadhorotesha ufanisi.

Aidha wananchi wameombwa kutoa ushirikiano kwa Serikali, kwa kua wazalendo na kuacha vitendo vya uhujumu wa zoezi hilo muhimu na badala yake kua walinzi wa vifaa ili kupata taarifa zitakazoleta majibu sahihi ya utafiti huo.

“Tunawaomba wananchi kuheshimu vifaa vya utafiti huu kwa kutovihamisha au kuviharibu ili kwa Pamoja kufanikisha utafiti huu muhimu kwa maendeleo ya nchi yetu” amesema Mhe. Sufiani